Karibu OCP Afrika
Triple Super Phosphate (TSP)
Kwa kilimo endelevu
Kwanini utumie mbolea ya TSP?
Hifadhi ya Kirutubisho cha Fosiforasi Kurejeshwa Tena
Mazao hukumbana na upungufu mkubwa wa kirutubisho cha fosiforasi, kutokana na udongo kutokuwa na kiwango cha kutosha cha fosiforasi , kilimo kisichozingatia mbinu nzuri na ardhi kulimwa kwa muda mrefu na kupelekea kuvunwa kwa fosiforasi bila kurejeshwa. TSP hurejesha kirutubisho hiki muhimu (fosiforas) kwenye udongo na kuuhakikishia mmea uotaji, ustawi na uzalishaji mzuri na wenye tija kwa mazao yote.
Kiwango Kikubwa cha Fosiforus
Mbolea ya TSP ina asilimia 46 ya fosiforasi (P205), hupatikana kirahisi, na kuzalisha mizizi mingi na mirefu inayopelekea ukuaji mzuri wa mmea.
Iliyotengenezwa Kukidhi Mahitaji
Imesheheni madini kukidhi mahitaji ya mmea kwa kiwango na wakati sahihi.
Gharama Nafuu
Huboresha matumizi ya kirutubisho na kupunguza upotevu wa fosiforasi na kulinda thamani ya uwekezaji wako.
Usimamizi wa Virutubisho - 4R
Chanzo Sahihi
Mbolea ya TSP ina kiwango kikubwa cha kirutubisho cha fosiforasi, hutumika wakati wa kuotesha na hufanya vizuri kwenye udongo wenye tindikali/asidi
Mahali Sahihi
Weka mbolea ya fosiforasi karibu na mizizi ili kuboresha ufanisi(sentimita 5 chini au pembeni ya mbegu/mmea). Ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi mbolea ya TSP imetengezwa kwa punje zilizo sawa na zenye kufanana.
Wakati Sahihi
Fosiforasi ni muhimu kuwekwa mwanzoni ili kusaidia ukuajia wa mizizi na mmea.
Kiasi Sahihi
Kuongeza mavuno tumia kiwango sahihi cha mbolea ya TSP kama inavyoshauriwa.
Kwanini Utumie Virutubisho Kijalizi
Husaidia kilimo endelevu kwa athari ndogo kwa mazingira. Pia hupunguza kupotea kwa virutubisho na mtiririko wa maji. Kumbuka: Mbolea ya TSP hutumika kuoteshea mazao yote